Akiba ya fedha za kigeni nchini China yafikia USD trilioni 3.25 mwishoni mwa Disemba mwaka jana
2022-01-10 08:15:53| CRI

Takwimu kutoka mamlaka ya usimamizi ya fedha za kigeni ya China zinaonyesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2021, akiba ya fedha za kigeni nchini China imefikia dola za kimarekani trilioni 32.502, ikiongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 27.8 ikilinganishwa na mwishoni mwa mwezi Novemba.

Mamlaka hiyo imesema, akiba ya fedha za kigeni imeongeza kwa miezi mitatu mfululizo, na kufikia kiwango cha juu tangu mwaka 2016.

Naibu mkuu wa mamlaka hiyo ambaye pia ni msemaji wa mamlaka hiyo Bibi Wang Chunying amesema, China imeratibisha kazi za kinga na udhibiti wa maambukizi ya COVID-19 huku ikihimiza maendeleo ya jamii na uchumi. Amesema uchumi wa China umekuwa na unyumbufu mkubwa, hali ya kimsingi ya mwelekeo mzuri wa uchumi haijabadilika, na inasaidia utulivu wa jumla wa akiba ya fedha za kigeni.