Mali yatangaza kufunga mipaka ya ardhi na ya anga na nchi jirani za ECOWAS
2022-01-11 08:21:13| cri

 

Serikali ya mpito ya Mali jana imetangaza kuwa itafunga mipaka ya nchi kavu na ya anga ya pamoja na nchi jirani za Jumuiya ya Kiuchumu ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), na kurudisha mabalozi wake katika nchi wanachama wa ECOWAS, ili kujibu vikwazo vilivyowekwa na Jumuiya hiyo dhidi yake.

Baada ya mkutano maalumu uliofanyika jumapili mjini Accara, Ghana, viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS walitoa taarifa ya pamoja wakisema, Jumuiya hiyo imeamua kudumisha vikwazo vilivyowekwa awali dhidi ya serikali ya mpito ya Mali, vilevile kuongeza vikwazo vipya, kutokana na serikali ya mpito ya Mali kushindwa kukamilisha mpito wa siasa kabla ya mwezi Februari mwaka huu.