Iran yakanusha kufikia mkataba wa muda katika mazungumzo ya suala la nyuklia
2022-01-11 08:25:52| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bw. Saeed Khatibzadeh amesema, nchi hiyo imeondoa uwezekano wa kufikia "makubaliano ya muda" katika mazungumzo ya suala la nyuklia la Iran ambayo hayakidhi matakwa ya nchi hiyo.

Bw. Khatibzadeh pia amesema, pande zote zinapaswa kujitahidi kupata uhakikisho na uthibitisho unaohitajika kwa Marekani kurejea kwenye mazungumzo hayo, na kuhakikisha kwamba vikwazo dhidi ya Iran vinaondolewa kikamilifu. Na hayo hayawezi kutimizwa kupitia makubaliano ya muda, hivyo Iran inatafuta makubaliano yasiyobadiliki na ya kutegemeka.