Ziara ya Wang Yi kuhimiza zaidi ushirikiano kati ya China na Kenya
2022-01-12 09:32:13| CRI

Ziara ya Wang Yi kuhimiza zaidi ushirikiano kati ya China na Kenya_fororder_微信图片_20220110104924

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hivi karibuni alipohudhuria hafla ya kumalizika kwa mradi wa bandari ya mafuta ya Mombasa uliojengwa na kampuni ya China pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyekuwa ziarani nchini humo, amesema Kenya na Afrika zinahitaji marafiki wanaopenda kushirikiana nao kutimiza malengo. Amepongeza China kwa kuiunga mkono Kenya kupata maendeleo, na ni rafiki kweli wa Kenya.

Kama reli ya SGR, bandari ya mafuta ya Mombasa ni mradi mwingine muhimu ya kustawisha uchumi wa Kenya. Baada ya kuzinduliwa, bandari hiyo mpya itasaidia nchi hiyo kuokoa shilingi bilioni 2 za Kenya sawa na zaidi ya dola milioni 17 za Kimarekani kwa mwaka. 

Kuanzia tarehe 4 hadi 7 mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitembelea nchi tatu za Afrika za Eritrea, Kenya na Comoro. Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea Afrika mwanzoni mwa mwaka mpya ni desturi iliyoendelea kwa miaka 32 ya China. Kenya ni kituo muhimu cha ziara hiyo.

Kwenye mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), rais Xi Jinping wa China alitangaza mapendekezo muhimu ya kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili ikiwemo “Miradi 9”. Lengo kuu la ziara ya Wang Yi ni kutekeleza matokeo ya mkutano huo, na kuziunga mkono nchi za Afrika kushinda janga la COVID-19 na kufufua uchumi mapema.

Hadi sasa kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika zimezidi milioni 10, lakini kiwango cha watu waliochanjwa hakijafikia asilimia 10, hivyo Afrika inahitaji sana chanjo dhidi ya COVID-19. Kwenye mkutano wa FOCAC uliofanyika nchini Senegal, China iliahidi kutoa dozi nyingine bilioni moja kwa nchi za Afrika. Wakati Wang alipotembelea Kenya, alisema China itatoa dozi nyingine milioni 10 za chanjo kwa Kenya, na kusisitiza kuwa, China itakuwa pamoja na ndugu zake wa Afrika mpaka zipate ushindi wa mwisho.

Katika ziara yake barani Afrika, Wang alisaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano na Kenya katika sekta za uchumi wa kidijitali, uwekezaji na kilimo. China itaunga mkono Kenya kuanzisha eneo la kiuchumi kando ya reli ya SGR, na kuisaidia Kenya kutumia vizuri “njia rahisi” ya kuuuza China bidhaa za mazao ya kilimo.

Alipotembelea nchini Kenya, Wang pia ametangaza kuwa China itateua balozi maalumu anayeshughulikia mambo ya Pembe ya Afrika, ili kutoa mchango zaidi katika kulinda amani na usalama barani Afrika.

Reli zaidi ya kilomita 10, barabara karibu laki moja, madaraja karibu elfu moja, bandari karibu mia moja, na hospitali na shule nyingi, matokeo hayo ya ushirikiano kati ya China na Afrika yamenufaisha watu wa Afrika. Rais Uhuru amesema China ina nia dhati ya kuisaidia Afrika kutatua masuala.