Afrika Mashariki yatakiwa kuongeza utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19
2022-01-12 08:18:29| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imewataka watu wa kanda hiyo kujitokeza kwa wingi kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona kama sehemu ya juhudi za pamoja za kudhibiti kuenea kwa virusi katika kanda hiyo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana jijini Nairobi, Kenya, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Peter Mathuki pia amewataka wale waliopata chanjo kupata chanjo ya nyogeza ili kuhakikisha kinga endelevu dhidi ya virusi hivyo.

Amesema pingamizi dhidi ya kupata chanjo hizo inarudisha nyuma juhudi za kufufua uchumi wa kanda hiyo baada ya athari zilizotokana na janga hilo, na kuongeza kuwa, dunia inapoelekea sasa, itakuwa ni lazima kwa wasafiri na wanaohudhuria mikutano kuonyesha cheti kinachothibitisha kuwa wamepata chanjo ya COVID-19.