Benki ya Dunia yapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi duniani mwaka 2022 hadi asilimia 4.1
2022-01-12 08:17:36| CRI

Benki ya Dunia yapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi duniani mwaka 2022 hadi asilimia 4.1_fororder_timg (41)

Benki ya Dunia jana ilitangaza ripoti mpya ya makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia ikisema, uchumi wa dunia kwa mwaka 2021 unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5.5, na ongezeko hilo la mwaka 2022 litafikia asilimia 4.1 ambayo ni pungufu kwa asilimia 0.2 kuliko makadirio ya awali.

Ripoti hiyo inasema, kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona yanayoendelea kuenea, kupungua kwa nguvu za sera za nchi mbalimbali na kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya mlolongo wa ugavi, mwelekeo wa ufufukaji wa uchumi duniani umepungua. Pia uzalishaji katika masoko yanayoibuka na makundi ya uchumi yanayoendelea unakadiriwa kupungua chini ya kiwango cha kabla ya maambukizi ya COVID-19.