Rais wa China atoa wito wa kufahamu na kutumia vizuri zaidi uzoefu wa CPC
2022-01-12 08:19:57| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amehutubia ufunguzi wa Semina ya Maofisa wa Ngazi ya Mikoa na Wizara, akiwataka kufahamu na kutumia vizuri zaidi uzoefu wa miaka 100 wa CPC, na kuendelea na juhudi kwa ajili ya kutimiza Lengo la pili la Mwaka 100.

Rais Xi amesema, hivi sasa dunia na China inakabiliwa na mabadiliko ya kasi, na CPC inapaswa kuwa mbele zaidi ya maendeleo ya binadamu, kusikiliza vizuri matarajio ya watu wa China na kukidhi mahitaji yao. Pia amesema Chama hicho kinapaswa kukomboa mawazo, kufuata ukweli, kufanya uvumbuzi, na kuendelea kuunganisha nadharia ya Umaksi na hali halisi ya China na utamaduni wa China.

Rais Xi pia amewahimiza maofisa hao kuongeza juhudi katika kupambana na ufisadi.