Watu 10 wauawa na wengine 9 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu nchini Somalia
2022-01-13 08:28:09| cri

Watu 10 wauawa na wengine 9 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu nchini Somalia_fororder_d50735fae6cd7b8945ba8c1fc1d2faaedb330e5c

Polisi nchini Somalia jana wamesema, watu 10 wameuawa wakiwemo wanajeshi watano na wengine 9 kujeruhiwa baada ya gari lilotegwa mabomu kulipuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Polisi pia wamesema, shambulizi hilo lililenga msafara uliokuwa ukisindikiza wageni kwenye barabara kuu karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa, na uchunguzi unaendelea.

Habair zinasema, kundi la al-Shabaab nchini Somalia limekiri kuhusika na shambulizi hilo.