China yatimiza lengo la kushirikisha watu milioni 300 katika michezo ya majira ya baridi
2022-01-13 08:31:43| CRI

China yatimiza lengo la kushirikisha watu milioni 300 katika michezo ya majira ya baridi_fororder_VCG111362170386

China imetimiza ahadi yake ya kushirikisha watu milioni 300 katika michezo ya majira ya baridi.

Takwimu zilizotolewa jana jumatano na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonyesha kuwa, zaidi ya Wachina milioni 346 wameshiriki katika shughuli za michezo ya majira ya baridi tangu mwaka 2015 wakati Beijing iliposhinda kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2022.

Michezo hiyo imepata umaarufu kwa vijana, kutokana na asilimia 82 ya washiriki kuwa na umri wa kati ya miaka 18 hadi 30, wakichukua asilimia 37.27 ya idadi ya jumla ya watu nchini China.

Kati ya watu hao milioni 346, milioni 143 wanaishi mashariki mwa China, milioni 51 kutoka kaskazini mashariki, milioni 84 kutoka magharibi na milioni 68 wanatokea katikati ya China.