Uchumi wa dunia kwa mwaka 2022 wakadiriwa kukua kwa asilimia 4
2022-01-14 08:08:28| CRI

Ripoti ya Mazingira na Matarajio ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema, uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa asilimia 4 mwaka 2022 na asilimia 3.5 mwaka ujao.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana imesema, ufufukaji wa uchumi wa dunia unakabiliwa na hali ngumu kutokana na wimbi jipya la maambukizi ya COVID-19, kuendelea kuwepo kwa changamoto katika soko la ajira, na changamoto katika mnyororo wa ugavi pamoja na shinikizo la kuongezeka kwa gharama za vyakula.

Katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amesema, huu ni wakati wa kuondoa pengo la ukosefu wa usawa ndani na kati ya nchi mbalimbali, na kuongeza kuwa, kwa kushirikiana, inawezekana kuufanya mwaka huu wa 2022 kuwa mwaka ya ufufukaji wa maisha ya watu pamoja na uchumi.