Haini - Shafi Adam
2022-01-14 14:39:08| cri

Haini - Shafi Adam_fororder_80c6173a51eb9df7c699c86af84bb01

Riwaya ya Haini ya Shafi Adam Shafi, inapania kudhihirisha jinsi maudhui ya jamii ya kigereza yanavyobainika kuambatana na sifa zinazotambuliwa na Michael Foucault ambaye ni mwasisi wa nadharia ya Ki-Foucault inayoongoza uhakiki huu. Aghalabu msanii wa fasihi anachota malighafi yake kutokana na jamii anamokulia pamoja na tajriba yake inayoongozwa na ubunifu wake. Pia, matukio na asasi mbalimbali za jamii hutoa mchango mkubwa katika kuendeleza maudhui katika fasihi ya Kiswahili. Gereza ni mojawapo ya asasi zinazokuwa chemichemi ya maudhui yanayoendeleza fasihi katika jamii.