AfCFTA na wenzi wake wazindua utaratibu wa malipo ya kuvuka mpaka ili kuboresha maingiliano ya biashara Afrika
2022-01-14 08:07:57| CRI

Sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA), Benki ya Afrexim, na wenzi wengine wamezindua Utaratibu wa Malipo na Mapatano wa Afrika (PAPSS) kwa lengo la kuboresha maingiliano ya biashara barani Afrika.

Uzinduzi huo uliofanyika jana, ulifuatiwa na mafanikio ya majaribio ya mfumo huo katika nchi sita za Ukanda wa Kifedha wa Afrika Magharibi ambazo ni Ghana, Nigeria, Gambia, Liberia, Guinea na Sierra Leone.

Akizundua mfumo huo, rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia amesema, PAPSS itamaliza utegemezi wa Afrika kwa sarafu ya upande wa tatu kwa ajili ya malipo, na kusaidia kuinua biashara ya ndani ya Afrika ili kuchochea mageuzi ya kiviwanda na kuinua ukuaji endelevu na jumuishi wa uchumi barani Afrika.

Naye Katibu Mkuu wa AfCFTA Wamkele Mene amesema, uzinduzi wa mfumo huo umefanyika kwa wakati na utaboresha kihalisi biashara ya ndani ya Afrika kwa kufanya malipo ya kuvuka mpaka kuacha kutegemea sarafu ya upande wa tatu.