Utengano –Said A. Mohamed
2022-01-14 14:40:12| cri

Utengano –Said A. Mohamed_fororder_图像_2022-01-14_144005


Riwaya hii inaeleza haswa kuhusu uozo katika ndoa, siasa, dini na jamii kwa jumla. Kupitia utengano wa kifamilia Mhusika mkuu Maimuna anatoroka kutoka kwa babake Mzee Maksudi, wanaomsaidia Maimuna kutoroka ni wale walioteswa na kudhulumiwa na Maksudi. Hii ndio njia ya pekee kwao kumtenda Bwana Maksudi. Kimaksudi wanaisambaratisha familia yake na kumzamisha bintiye katika ukahaba na ulevi wa kupindukia. Kupitia kwa vimbwanga na mateso ya Maimuna, utengano wa kiuchumi baina ya matajiri na maskini unadhihirika wazi, utengano wa kifamilia, ndoa, utengano wa kikazi pia unaonekana wazi bila kusahau unafiki na utengano wa kidini miongoni mwa wahusika.