China yalaumu kitendo cha kufuja chanjo ya COVID-19
2022-01-14 08:29:33| CRI

China yalaumu kitendo cha kufuja chanjo ya COVID-19_fororder_汪文斌

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, wakati maambukizi ya COVID-19 yanaendelea duniani, huku virusi vipya vilivyobadilika vikiendelea kugunduliwa, kitendo cha kufuja chanjo cha baadhi ya nchi kinapaswa kulaumiwa.

Habari zinasema, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus hivi karibuni amesema, zaidi ya nchi 90 hazijatimiza lengo la kuchanja asilimia 40 ya watu wao, ambapo zaidi ya asilimia 85 ya watu barani Afrika hawajapata dozi ya kwanza ya chanjo.

Wang amesema, China daima inaona kuwa kupambana na janga la COVID-19 ni jukumu la pamoja la nchi zote, na chanjo ni silaha kuu dhidi ya janga hilo, lakini pengo la upatikanaji wa chanjo kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea bado linaongezeka. Ameongeza kuwa, kati ya watu bilioni 1.3 barani Afrika, ni asilimia 7.5 tu wamepata chanjo kamili, wakati huo huo baadhi ya nchi za magharibi zinalimbikiza chanjo kuzidi mahitaji yao, na kusababisha ufujaji mkubwa.