Kremlin: Majeshi ya Russia kuwekwa karibu na mpaka wa Ukraine kufuatia shinikizo la NATO
2022-01-17 10:50:57| CRI

Kremlin: Majeshi ya Russia kuwekwa karibu na mpaka wa Ukraine kufuatia shinikizo la NATO_fororder_俄罗斯

Msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin, Dmitry Peskov amesema Russia itaweka wanajeshi wake katika eneo lake karibu na mpaka wa Ukraine kutokana hali ya wasiwasi na mazingira yasiyo rafiki ya Jumuiya ya Kujihami NATO.

Amesema lazima Russia ichukue hatua za tahadhari ikijibu mazoezi ya kijeshi, luteka na safari za ndege za mara kwa mara za NATO karibu na mipaka ya Russia. Hata hivyo amesisitiza kuwa Russia haifikirii hatua za kijeshi hata kama mazungumzo na Marekani na NATO juu ya uhakikisho wa kiusalama yameshindwa.

Mapema wiki iliyopita wanadiplomasia wa Russia walifanya mazungumzo na Marekani huko Geneva, pia na Shirika la Usalama na Operesheni za pamoja la Ulaya huko Vienna halafu walifanya na NATO huko Brussels. Mazungumzo yote hayo yaliisha bila mafanikio yoyote.