UNHCR: mgogoro wa Sahel wasababisha watu milioni 2.5 kukimbia makazi
2022-01-17 10:56:00| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuratibu hatua ili kukomesha mgogoro katika ukanda wa Sahel, katikati ya Afrika, ambao umesababisha watu milioni 2.5 kukimbia makazi katika miaka kumi iliyopita.

UNHCR na washirika wake wa kibinadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kutoa misaada na kulengwa katika mashambulizi pamoja na kutekwa kwa magari yao.

UNHCR pia imesema dola za kimarekani milioni 307 zinahitajika mwaka huu ili kuchukua hatua zenye ufanisi katika nchi za Burkina Faso, Niger na Mali.