UM na mashirika mbalimbali yafanya maandalizi ya uokoaji baada ya kulipuka kwa volcano ya Tonga
2022-01-18 10:21:16| CRI

UM na mashirika mbalimbali yafanya maandalizi ya uokoaji baada ya kulipuka kwa volcano ya Tonga_fororder_汤加

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana alisema umoja huo na mashirika yake wanafanya maandalizi ya uokoaji baada ya volkano ya Hunga Tonga-Hunga Ha'apai kulipuka katika kisiwa cha Tonga.

Dujarric amesema habari kutoka kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na serikali zimesema miundombinu muhimu imeharibiwa vibaya katika eneo la kisiwa kikuu cha Tongatapu, na hakuna mawasiliano na Visiwa vya Ha'apai. Visiwa vidogo viwili vya Mango na Fonoi vinafuatiliwa zaidi kutokana na hasara kubwa ya mali.

Amesema mashirika mbalimbali yamefanya kazi ya maandalizi ya uokoaji, ikiwa ni pamoja na Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP), Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), na Shirika la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) .