Rais Xi atoa hotuba maalumu kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani la mwaka 2022
2022-01-18 10:22:05| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumatatu alitoa hotuba maalumu kwenye Baraza la Uchumi Duniani la mwaka 2022.

Kwenye hotuba yake ambayo imesheheni mapendekezo na ahadi mbalimbali, rais Xi kwanza alizungumzia kuhusu mwaka mpya wa jadi wa China “Mwaka wa Chui Milia” ambao utasherehekewa baada ya wiki mbili na kusema kwamba mwaka huu ukiwa unaashiria ushujaa na ujasiri kwa utamaduni wa China, hivyo ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazowakabili binadamu, tunapaswa kumuongezea “mbawa chui milia” na kuwa na ujasiri na nguvu kama za chui milia ili kuondokana na vizuizi vyote vilivyopo njiani wakati tukisonga mbele.

Akitaja mapendekezo hayo rais Xi amesema kwanza tunahitaji kukumbatia ushirikiano na kushinda kwa pamoja janga la COVID-19. Amesema kujiamini na ushirikiano ndio njia pekee iliyo sahihi ya kulinda janga na kwamba kurejeshana nyuma na kulaumiana kutasababisha uchelewashaji tu usiohitajika katika kupambana na kutuzia kutimiza malengo yetu.

Kwa pendekezo la pili rais Xi amesema tunahitaji kuondoa hatari mbalimbali na kuhimiza ufufukaji wenye utulivu wa uchumi wa dunia. Tatu alisema tunahitaji kuziba pengo la mgawanyiko wa maendeleo na kufufua maendeleo duniani. Na nne alisema tunahitaji kuondokana na mawazo ya vita baridi na kuishi pamoja kwa amani na kuleta matokeo ya kunufaishana.

Mbali na mapendekezo hayo, kwenye hotuba yake rais Xi pia aliahidi kwamba China itaendeleza dhamira yake ya kutafuta maendeleo ya hali ya juu, pia itaendeleza dhamira yake ya mageuzi na ufunguaji mlango, na kuendeleza dhamira yake ya kuhimiza uhifadhi wa kiikolojia.

Mwisho rais Xi aligusia Michezo ya Olimpiki na kusema Davos inajulikana kama pepo ya michezo ya baridi. Na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 pamoja na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu itafanyika hivi karibuni, hivyo Wachina wanaamini kwamba China itaipa dunia michezo myepesi, salama na mizuri. Kuhusu kauli mbiu ya michezo hii ambayo ni “Pamoja kwa Hatma ya pamoja”, rais Xi amesisitiza kuwa watu wanapaswa kushikana mikono huku wakijiamini, na kushirikiana pamoja kwa ajili ya hatma ya pamoja.