Mkuu wa UM atoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kidiplomasia kuhusu kutokomeza silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea
2022-01-18 10:26:26| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Korea Kaskazini na pande zote zinazohusika ili kutokomeza silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea.

DPRK iliripotiwa kurusha makombora mawili ya masafa mafupi katika bahari ya mashariki siku ya Jumatatu, ukiwa ni urushaji wa nne kufanyika katika chini ya wiki mbili.