Rais Xi asisitiza utawala kamili wa chama na kuahidi kutovumilia ufisadi
2022-01-19 09:37:09| CRI

Rais Xi asisitiza utawala kamili wa chama na kuahidi kutovumilia ufisadi_fororder_11

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC jana Jumanne alisisitiza kufanya juhudi kubwa na bila kuyumba na ili kuhimiza zaidi utawala kamili na mkali wa Chama.

Wakati akihutubia kikao cha sita cha Kamati kuu ya 19 ya Usimamizi na Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, Xi ambaye pia ni rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi, ameahidi kuendelea kutovumilia msimamo wa ufisadi. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning na Han Zheng wamehudhuria mkutano huo, ambapo  Han Zheng pia aliongoza mkutano.

Tangu Baraza la Taifa la 18 la CPC la mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC imeboresha maadili ya chama, kushikilia uadilifu na kupambana na ufisadi kwa ujasiri mkubwa.