Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing
2022-01-19 08:16:05| CRI

Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing

Kongamano maalumu kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lilifanyika jana tarehe 18 katika Ubalozi wa Ethiopia nchini China. Kongamano hilo lenye kaulimbinu “Kuelekea Kwa Pamoja Siku Zijazo zilio Kijani Zaidi, zenye Ustawi na Afya Zaidi”, limeandaliwa kwa pamoja na Jopo la mabalozi wa nchi za Afrika nchini China na Ofisi ya Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China.

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wu Peng alishiriki na kuhutubia kongamano hilo kwa njia ya video, ambapo ameelezea matunda makuu yaliyopatikana katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC na hali ya utekelezaji wa matokeo hayo katika muda wa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kufanyika.

Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing

Bw. Wu Peng amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika ni ushirikiano wa Kusini-Kusini, na pia ni ushirikiano wa kirafiki kati ya ndugu. China siku zote inatoa misaada yake kadri iwezavyo kwa nchi za Afrika kulingana na nia ya nchi hizo, na itafanya kila juhudi kuongeza ubora na kuinua ufanisi wa ushirikiano wa China na Afrika. Bw. Wu Peng ameeleza matumaini yake kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yataimarisha uratibu katika kuchochea maendeleo ya kilimo, kuendeleza juhudi za kupunguza umaskini na kuhimiza maendeleo ya makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati barani Afrika, ili kusukuma mbele kwa pamoja maendeleo ya uchumi na jamii katika nchi za Afrika, na kuiunga mkono Afrika kwenye safari yake ya kuelekea siku zijazo za kijani zaidi, zenye ustawi na afya zaidi.

Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing

Akihutubia kongamano hilo, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Siddharth Chatterjee amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika unasaidia kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia nzima. China sasa imekuwa uchumi mkubwa wa pili duniani, na Afrika ina mustakbali mkubwa katika idadi ya watu, matibabu na uchumi wa kijani na kibuluu, hasa katika sekta ya kilimo ya Afrika, ambayo thamani yake inatarajiwa kufikia dola trilioni moja za kimarekani ifikapo mwaka 2030, na Afrika inakadiriwa kuwa soko kubwa zaidi duniani ifikapo mwaka 2050. Bw. Chatterjee amesema, Umoja wa Mataifa unaziunga mkono China na Afrika kuungana kwa uwezo na raslimali, na unapenda kutoa kichocheo na kuhimiza ushirikiano mwingi zaidi kati ya pande hizo mbili.

Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing

Kaimu mkuu wa Jopo la Mabalozi wa Afrika nchini China, balozi wa Djibouti nchini China Bw. Abdallah Abdillahi Miguil amesema, mfumo wa ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa ni msukumo mkuu wa kuhimiza maendeleo ya bara zima la Afrika, na pia unachukua nafasi muhimu katika utimizaji wa Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika. Balozi Miguil ameishukuru China kwa kuchangia uzoefu wake kwa nchi za Afrika kwenye sekta ya uchukuzi wa kuvuka mipaka na biashara ya mtandao, kuisaidia Afrika kujenga kituo cha ugavi cha biashara ya mtandao, na kutoa msaada kwenye ujenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika. Anatarajia kuwa katika siku zijazo Afrika na China zitaimarisha zaidi ushirikiano kwenye uzalishaji wa dawa na vifaa tiba, uchakataji, uhifadhi na usafirishaji wa mazao ya kilimo na utoaji mikopo kwa kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati, na kutekeleza kwa pamoja matunda yaliyopatikana katika mikutano ya FOCAC, ili kunufaisha watu wa China na Afrika.

Kongamano kuhusu kazi zijazo za Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC lafanyika Beijing

Maofisa wa serikali ya China, mabalozi wa nchi za Afrika, wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Kamati ya Umoja wa Afrika, wajumbe kutoka mashirika ya kifedha, mashirika yasiyo ya kiserikali na jumuiya za washauri bingwa zaidi ya 130 walishiriki kwenye kongamano hilo.