Kenya yaahidi kuimarisha utaratibu wa pande nyingi na mapendekezo ya amani ya kikanda
2022-01-19 09:36:13| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuwa serikali ya Kenya itaimarisha hatua za pande nyingi juu ya kupunguza mabadiliko ya tabianchi na kuongoza amani na usalama wa kikanda.

Akiongea kwenye tafrija aliyomuandalia mgeni wake rais wa Hungary Janos Ader aliyepo ziarani nchini Kenya juzi Jumatatu usiku, rais Kenyatta amesema kupunguza mabadiliko ya tabianchi ni jambo muhimu kwa sasa, serikali yake inaahidi kuifanya kazi hiyo muhimu ihusiane na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linafuatilia sana masuala ya tabianchi na usalama.

Pia amesisitiza tena ahadi ya Kenya juu ya utaratibu wa pande nyingi, nchi ambayo inaunga mkono kikamilifu mfumo wa Umoja wa Mataifa. Kenya itatumia uzoefu wake wa upatanishi wa amani katika kuunga mkono utulivu endelevu wa Afrika hasa kwa eneo la Pembe ya Afrika.