Xi Jinping atuma salamu za pole kwa Mfalme wa Tonga
2022-01-20 10:04:06| CRI

Januari 19, Rais Xi Jinping wa China jana amemtumia salamu za pole Mfalme Tupou VI wa Tonga kwa nchi ya Tonga kukumbwa na maafa makubwa yaliyosababishwa na mlipuko wa volcano.

Xi amesema ameshtushwa na mlipuko wa volcano kusababisha maafa makubwa na tsunami nchini Tonga, hali ambayo imeleta  hasara kubwa.  Akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, na yeye mwenyewe, ametoa salamu za pole kwa serikali ya Tonga na watu wake . China na Tonga ni wenzi wa kimkakati wa pande zote wanaoungana mkono na kusaidiana. China inapenda kutoa msaada kwa  Tonga kadri iwezavyo, ili kuwasaidia wananchi wa Tonga kushinda maafa na kujenga upya maskani yao .

Wakati huohuo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametuma salamu za pole kwa mwenzake wa Tonga Bw. Siaosi Sovaleni.