Mazoezi ya pili ya Tamasha la Sikukuu ya Spring la mwaka 2022 yafurahisha watu
2022-01-23 20:38:22| Cri

Januari 23, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limefanya mazoezi ya pili ya Tamasha la Spring la mwaka 2022, ambayo yameleta mambo mengi ya kufurahisha watu.

Tamasha hili la mwaka huu linalojumuisha programu mbalimbali za lugha, nyimbo, dansi, opera za kitamaduni, pamoja na sarakasi na magic, zitaleta mambo mengi yenye maana na kuvutia watu, na kujitahidi kuonesha mabadiliko ya maendeleo yaliyopatikana katika zama mpya.