Wanawake wa China na Afrika wanavyosherehekea mwaka mpya wa jadi wa China
2022-01-24 14:55:48| Cri

China sasa ipo kwenye maandalizi ya kuukaribisha mwaka mpya wa jadi wa China, ambapo mwaka huu tunaita mwaka wa Chuimilia. Hivi sasa ukipita mitaani utaona hali na mazingira yalivyobadilika kwani barabarani kumepambwa taa nyekundu, watu wameshaanza kubandika karatasi za kutakiana baraka mlangoni, na pia wachina wanapilikapilika za kununua vyakula mbalimbali kwa ajili ya kupika katika kipindi hiki cha sikukuu.

Tunafahamu kuwa katika kipindi hiki mwanamke anakuwa mbelembele kufanya maandalizi mengi tu ili kuhakikisha sikukuu inakuwa nzuri, na familia inapata kufurahi pamoja kwa kula na kunywa na pia kuvaa vizuri. Lakini mwanamke nafasi yake sio jikoni pekee, bali ana majukumu mengi ya kijamii anayoshiriki kwani kwa mara ya kwanza wanaanga wa China mwaka huu wanasherehekea katika anga za juu, na miongoni mwao yuko mwanaanga mwanamke. Kwa hiyo leo hii katika ukumbi wa wanawake mbali na kusikia mwanamke anayesherehekea mwaka mpya akiwa anga za juu pia tutasikia wanawake wengine wenyeji na wageni wakiuelezea mwaka wa jadi wa China unavyosherehekewa.