Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kati ya vijana duniani
2022-01-25 11:02:38| CRI

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema anaamini kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itapata mafanikio makubwa na kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kati ya vijana wa nchi mbalimbali zikiwemo Korea Kusini na China.

Kituo cha utafiti cha kitaifa cha Chuo kikuu cha mambo ya nje cha China siku hiyo kimefanya semina ya kimataifa kuhusu "Urafiki kati ya China na Korea Kusini na Ushirikiano wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi" mjini Beijing. Bw. Ban Ki-moon katika hotuba yake kwa njia ya video amesema kwamba wakati wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Korea Kusini na China, kuongeza maelewano kwa kupanua mawasiliano ya utamaduni na michezo kutaweka msingi imara wa urafiki, maelewano na kuaminiana kati ya vijana vya nchi hizo mbili.