Rais Xi Jinping aongoza mkutano wa uongozi wa CPC kupitia ripoti na kanuni
2022-01-25 09:11:21| CRI

Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China (CPC) na Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu aliongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya kamati kuu ya CPC.

Mkutano huo ulipitia ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa baada ya kamati hiyo kusikiliza na kujadili ripoti za kazi za vikundi vya makada viongozi katika kamati ya kudumu ya Bunge, Baraza la Serikali, Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, Mahakama Kuu, Idara Kuu ya Kuendesha Mashtaka, pamoja na ripoti ya kazi ya sekritarieti ya Kamati Kuu ya chama.

Kanuni kuhusu ushughulikiaji wa barua na ziara za kuwasilisha malalamiko pia ilipitiwa. Mkutano huo ulitambua kazi nzuri zilizofanywa na idara hizo katika mwaka 2021, na kupitisha mipango yao ya kazi kwa mwaka huu.