Mlipuko wa malaria watokea kusini magharibi mwa Botswana
2022-01-25 09:10:48| CRI

Mfumo wa huduma za afya nchini Botswana unakabiliwa na shinikizo kubwa zaidi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa malaria uliotokea hivi karibuni kwenye sehemu ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Mratibu wa timu ya usimamizi wa afya kwenye eneo hilo Nthabiseng Dikgang, amesema watu wasiopungua 11 wamethibibithwa kuambukizwa malaria katika miezi mitatu iliyopita kwenye eneo hilo, ambalo halikushuhudia maambukizi ya ugonjwa huo katika historia.

Dikgang amehimiza umma kufuatilia dalili za malaria na kutafuta matibabu haraka iwezekanavyo, ili kuepuka maambukizi mabaya na hata vifo.