CMG yafanya mazoezi ya tatu ya Tamasha la Sikukuu ya Spring la mwaka 2022
2022-01-25 21:48:27| Cri

Mazoezi ya tatu ya Tamasha la Sikukuu ya Spring la mwaka 2022 la Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) yamefanyika leo .

Tamasha hilo la mwaka huu linazingatia mambo halisi ya kugusa mioyo ya watu, ambalo linajumuisha programu zinazoonesha utamaduni wa jadi, ustawishaji wa vijiji, ustaarabu wa kiikolojia na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Tamasha hilo litaoneshwa rasmi Januari 31, mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China.