Wanawake wana ufundi ama ujuzi wa aina mbalimbali wanaowasaidia katika kujikimu kimaisha na kusaidia kutelekeza majukumu kwenye familia. Wanawake wengi wanajihusisha na sekta isiyo rasmi, kama vile utengenezaji wa vikapu, sabuni, ushonaji na hata mapishi. mambo haya yote yanawasaidia kujiongezea kipato na kusaidia malezi na majukumu ya kutunza familia. Katika kipindi cha leo tunazungumzia wanawake wabunifu katika sanaa za mikono, ikiwemo ushonaji, ufumaji na upakaji wa hina.