Rais Xi Jinping asema China itaandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi iliyo salama na mizuri
2022-01-26 09:06:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China amemwamba mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) Bw. Thomas Bach ambaye yuko ziarani nchini China kwamba China itaandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi iliyo salama na mizuri.

Rais Xi alikutana na Bw. Bach jana mjini Beijing, siku kumi kabla ya ufunguzi rasmi wa Michezo hiyo utakaofanyika Februari 4.

Rais Xi amesema “kila kitu kiko tayari” kwa ajili ya michezo hiyo, ambayo itakuwa michezo ya kwanza ya kimataifa kufanyika kama ilivyopangwa tangu janga la virusi vya Corona lilipolipuka.

Kwa mujibu wa rais Xi, wanamichezo wapatao 3,000 kutoka nchi na sehemu 90 watashindana kwenye michezo hiyo.