IMF yapunguza makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2022 hadi 4.4%
2022-01-26 09:05:27| CRI

Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia iliyotolewa jana Jumanne na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF inakadiria kuwa uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 4.4 mwaka huu, ikipungua kwa asilimia 0.5 kuliko makadirio yaliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana.

IMF inaona hali ya uchumi ya mwaka huu ni dhaifu zaidi kuliko ilivyokadiriwa awali, kutokana na hatua mpya za zuio la usafiri zilizowekwa na nchi mbalimbali kufuatia mawimbi ya maambukizi ya virusi vilivyobadilika vya Omicron, kuendelea kupanda kwa bei ya nishati na kiwango cha juu cha mfumko wa bei unaosababishwa na kukatika kwa mnyororo wa ugavi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchumi wa China unakadiriwa kukua kwa asilimia 4.8 na asilimia 5.2 katika mwaka huu na mwaka kesho mtawalia.