Kongamano la kwanza la uvumbuzi wa vyombo vya habari duniani lafanyika Beijing
2022-01-27 09:11:24| CRI

Kongamano la kwanza la uvumbuzi wa vyombo vya habari duniani limefanyika jana Jumatano hapa Beijing. Mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa idara ya uenezi ya kamati hiyo Bw. Huang Kunming, amehudhuria ufunguzi wa kongamano hilo na kusoma barua ya pongezi kwa niaba ya Rais Xi Jinping.

Bw. Huang amesema barua ya pongezi ya Rais Xi imeonesha dhamira thabiti ya China kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, na kueleza matarajio kwa vyombo vya habari kuenzi moyo wa Olimpiki na kusukuma mbele maendeleo ya michezo ya majira ya baridi.