Tanzania na Morocco zaahidi kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji
2022-01-27 09:36:38| CRI

Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imetoa taarifa ikisema, Tanzania na Morocco zimeahidi kuimarisha uhusiano katika biashara na uwekezaji.

Taarifa hiyo imesema, nchi hizo mbili zimetoa ahadi hiyo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video kati ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bibi Liberata Mulamula na mwenzake wa Morocco Bw. Nasser Bourita.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nchi hizo mbili pia zimeahidi kuimarisha uhusiano katika sekta za elimu, utalii, uwezeshaji wa wanawake na vijana. Bibi Mulamula amesema, pande mbili zimekubali kupitia makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizo mbili wakati wa ziara ya mfalme wa Morocco nchini Tanzania mwaka 2016, na kuharakisha utekelezaji wa makubaliano hayo.