Wanafunzi zaidi ya 7,000 Msumbiji waathiriwa na dhoruba ya Ana
2022-01-27 09:23:30| cri

Radio ya Taifa ya Msumbiji imesema vyumba vya madarasa visivyopungua 64 katika jimbo la Nampula, kaskazini mwa nchi hiyo vimeharibiwa kwa viwango tofauti na dhoruba ya kitropiki Ana ambayo inawezekana kusababisha wanafunzi zaidi ya 7,000 kukosa madarasa ya kusomea katika mwaka mpya wa masomo.

Licha ya hayo nyumba za makazi zaidi ya 5,500 na miundombinu mingi ya barabara, madaraja na kituo kimoja cha afya katika jimbo hilo pia vimeharibiwa.

Waziri mkuu wa Msumbiji Carlos Agostinho do Rosario alipoongoza kikao cha Kamati ya Operesheni za Dharura amesema nchi hiyo inahitaji mpango mzuri zaidi wa kukabiliana na maafa yanayotokea mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.