Rais Xi Jinping apongeza kufunguliwa kwa baraza la CMG
2022-01-27 09:07:20| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa ufunguzi wa baraza la kwanza la Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lenye kauli mbiu ya “Pamoja kwa Olimpiki ya majira ya baridi ya teknolojia ya juu” linalofanyika mjini Beijing.

Rais Xi ameandika kwenye barua ya pongezi akisema anatumai kuwa washiriki wa bara hilo watachangia busara zao, ili kuleta uchangamfu kwenye michezo ya theluji na barafu, kuhimiza moyo wa Olimpiki na kuendeleza michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi.