Polisi Nigeria wakamata washukiwa 14 wa utekaji nyara
2022-01-28 08:48:21| CRI

Polisi nchini Nigeria wamesema jumla ya washukiwa 14 wa utekaji nyara wamekamatwa katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni katika jimbo la kaskazini la Jigawa.

Mkuu wa Polisi Jimbo la Jigawa Aliyu Tafida amewaambia wanahabari kuwa washukiwa hao walikamatwa jumatano baada ya askari polisi kuvamia maficho yao kwenye eneo moja la serikali jimboni humo.

Bw. Tafida amesema msichana mwenye umri wa miaka 20 aliyetekwa nyara Januari 8 aliokolewa bila kujeruhiwa kwenye operesheni hiyo.

Washukiwa hao, wakiwa ni wanaume kumi na wanawake wanne, watafunguliwa mashtaka mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.