Africa CDC: Nchi za Afrika zimefanya upimaji wa COVID-19 zaidi ya mara milioni 94
2022-01-28 08:47:28| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimesema, mpaka sasa nchi za Afrika zimefanya upimaji wa virusi vya Corona zaidi ya mara milioni 94.

Kituo hicho kimesema kiwango cha jumla cha matokeo chanya katika upimaji huo ni asilimia 11.3. Nchi tano, Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Misri na Ethiopia, zimechangia asilimia 60 ya maambukizi yote ya COVID-19 yaliyoripotiwa barani Afrika.