Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China lafanyika
2022-01-31 20:06:05| CRI

Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China lafanyika_fororder_春晚

Leo Tarehe 31 Januari mwaka 2022 ni siku ya mkesha kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa jadi kwa kalenda ya kilimo ya China, ambao rasmi unaingia tarehe Mosi Februari. Kwa utamaduni wa China, mwaka huu mpya utakuwa mwaka wa Chuimilia kwa mujibu wa mzunguko wa wanyama 12, ambapo kila mnyama anawakilisha mwaka mmoja, na kila baada ya miaka 12 mzunguko huo unajirudia.

Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China linaloandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG linafanyika leo usiku, ambalo litajumuisha maonesho kadhaa ya nyimbo na ngoma, maonyesho ya mazingaombwe na sarakasi na vipindi vingine vyenye uvumbuzi.

Kuanzia mwaka 1983, kituo cha taifa cha televisheni cha China CCTV kila ifikapo mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China kitaandaa kinaandaa tamasha la sanaa na utamaduni, liitwalo “Chunwan”. Wanafamilia wakikukusanya kukaa pamoja kutazama tamasha hilo, limekuwa desturi ya watu wa China.

Mwaka huu tamasha hilo kwa mara ya kwanza linatumia skrini ya LED kujenga kutengeneza kwenye paa lenye pembenukta nyuzi 720, na kutumia teknolojia ya XR na AR, teknolojia ya skani kwa pande zote na teknolojia ya 3D+4K. Vyombo vya habari zaidi 600 vya nchi na sehemu 170 duniani vitatangaza tamasha hilo moja kwa moja.