Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China laonyesha nia ya wachina katika safari mpya ya maendeleo ya zama mpya
2022-02-01 16:35:57| CRI

Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China laonyesha nia ya wachina katika safari mpya ya maendeleo ya zama mpya_fororder_微信图片_20220201163451

Saa 2 usiku wa tarehe 31 Januari, tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China lililoandaliwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG limerushwa hewani.

Tamasha hilo lilitumia skrini ya nyuzi 720 na teknolojia mbalimbali za XR, AR, ambalo limefuatiliwa na watazamaji na vyombo vya habari vya nchini na nje ya nchi.

Takwimu za awali zinaonyesha kuwa, hadi saa 6 usiku wa tarehe 31, Januari, kiwango cha wastani cha watu waliotazama tamasha hilo kwenye TV kimefikia asilimia 21.93, na idadi ya watazamaji kwenye vyombo vipya vya habari imefikia bilioni 4.932, kiasi ambacho kimeongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko mwaka jana. Na idadi ya watu wanaotazama tamasha hilo kwa njia ya simu imefikia milioni 200, zaidi ya asilimia 50 kati yao ni vijana chini ya umri wa miaka 30.

Vyombo vya habari zaidi 600 vya Marekani, Canada, Ufaransa, Italia, Russia, Japan, Brazil, India, Falme za Kiarabu (UAE), Afrika Kusini na nchi nyingine 170 wametangaza tamasha hilo moja kwa moja, na watu zaidi ya milioni 35.24 wa nchi za nje wametazama tamasha hilo kupitia CNTV na CGTN.