Mawaziri wa biashara wa Afrika watathmini maendeleo ya makubaliano ya biashara huria ya Afrika
2022-02-01 16:32:33| cri

Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) limekubali kuchukua hatua kuelekea kuanzisha biashara yenye maana chini ya eneo hilo.

Kwenye taarifa yake Sekretarieti imesema, baraza limekubali kwamba biashara chini ya AfCFTA inapaswa kuendelea chini ya msingi wa makubaliano ya sheria ya awali ambayo inasema ushuru unapaswa kuwa asilimia 87.7. Mkutano huo ulioitishwa Accra nchini Ghana katika wikiendi iliyopita, umeangazia hatua zilizofikiwa na taasisi za AfCFTA, ikiwa ni pamoja na Bodi ya Kusuluhisha Migogoro na Kuanzishwa kwa Bodi ya Rufaa.

Taarifa imesema katika huduma za biashara, mazungumzo yapo hatua nzuri, ambapo nchi wanachama 46 wamewasilisha ratiba zao za kuanza rasmi. Mawaziri wamesema mazungumzo juu ya huduma za biashara yatakamilika Juni 30.