WHO yapendekeza nchi kupunguza vizuizi vya hatua za kudhibiti COVID-19
2022-02-02 16:20:50| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limezitaka nchi zinazoanza kupunguza hatua za kudhibiti maambukizi ya COVID-19 kufanya hivyo kwa taratibu na kwa utulivu, kufuatia takwimu za karibuni kuonyesha kuongezeka kwa kasi kwa vifo vinavyotokana na virusi hivyo duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dr. Tedros Ghebreyesus amesema, tangu virusi vya Corona vilivyobadilika aina ya Omicron kugunduliwa wiki 10 zilizopita, karibu kesi milioni 90 zimeripotiwa katika Shirika hilo, ikiwa ni nyingi zaidi ya kesi zote zilizoripotiwa mwaka 2020.

Ameeleza wasiwasi wake juu ya mazungumzo yanayoendelea katika baadhi ya nchi kuwa kutokana na chanjo, na kwa kuwa virusi aina ya Omicron vinaambukiza kwa urahisi zaidi na havina madhara makubwa, hakuna tane ulazima wa kuzuia maambukizi. Amesema kuongezeka kwa maambukizi kunamaanisha kuongezeka kwa vifo, na kuzitaka nchi zote kulinda watu wake kwa kutumia vifaa vyote vinavyotakiwa, na si chanjo pekee.