Kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yafanya mkutano na waandishi wa habari
2022-02-02 16:27:07| CRI

Kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yafanya mkutano na waandishi wa habari_fororder_微信图片_20220202162939

Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing jana imefanya mkutano na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwafahamisha mambo yanayoingiliana na michezo hiyo na utamaduni wa jadi wa China.

Kwenye mkutano huo, video fupi imeonyeshwa kufahamisha desturi ya sikukuu ya Spring ya China na maana ya mwaka wa Chuimilia kwenye kalenda ya kilimo ya China, pia imeonyesha China iko tayari kuwapokea wageni kutoka nchi mbalimbali.

Maofisa wahusika pia wamesema ujenzi wa majumba ya michezo, alama, na ubunifu wa sanaa ya bustani umeingiza mambo mbalimbali ya utamaduni wa China.