Rais wa Marekani asema nchi yake iko tayari kuendeleza mawasiliano na Russia kuhusu masuala ya usalama
2022-02-02 16:21:18| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amemwambia mwenzake wa Russia Sergei Lavrov kuwa, Marekani iko tayari kuendeleza mawasiliano na Russia juu ya masuala ya kiusalama uanayozigusa pande hizo.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price imesema, Blinken amerejea tena ahadi ya Marekani kuhusu uhuru na mamlaka ya ardhi ya Ukraine, na pia haki ya nchi zote kuamua sera zao za kigeni na washirika wao.

Pia waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ameitaka Russia kupunguza mvutano katika mpaka wa Ukraine kwa kuondoa vikosi na vifaa vyake, na kusema Russia inapaswa kuchukua njia ya kidiplomasia katika kutatua mgogoro unaoendelea.