Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yamekamilika
2022-02-03 16:18:21| cri

Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yamekamilika_fororder_VCG111366651524

Mkurugenzi wa Idara ya Olimpiki ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, Bw. Pierre Ducre amesema, mpaka sasa, asilimia 70 ya wanariadha wamewasili Beijing na kufanya mazoezi katika uwanja na majumba mbalimbali.

Bw. Ducre amekuwepo mjini Beijing kwa muda wa mwezi mmoja akifanya shughuli mbalimbali za Kamati hiyo, na anasema ushirikiano wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa na Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni mzuri, na ameridhishwa sana na maendeleo yaliyopatikana.