Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na Rais Putin wa Russia
2022-02-04 19:14:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Russia_fororder_1128330630_16439728566651nRais Xi Jinping wa China leo alasiri amefanya mazungumzo na Russia Vladmir Putin wa Russia hapa Beijing, ambapo walibadilishana maoni kwa kina kuhusu uhusiano kati ya nchi zao, na masuala mbalimbali makubwa yanayohusiana na usalama na utulivu wa kimataifa.

Rais Xi amesisitiza kuwa, kwa sasa janga la maambukizi ya virusi vya korona linaendelea kuenea kote duniani, dunia imeingia kwenye kipindi cha msukosuko na mabadiliko, jamii ya binadamu inakabiliana na changamoto na hatari nyingi. Amesema anapenda kushirikiana na Rais Putin katika kuweka mustakabali wa uhusiano kati ya China na Russia chini ya hali mpya ya kihistoria, kuhimiza hali  juu ya kiwango cha kuaminiana kati ya nchi hizo mbili kuwa matokeo ya ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kunufaisha wananchi wao.

Rais Putin amesema Russia inapongeza mafanikio makubwa waliyopata wananchi wa China chini ya uongozi wa Chama cha CPC, na Russia inaichukulia China kuwa mwenzi wake muhimu zaidi wa kimkakati na rafiki yake mwenye nia ya pamoja, na uhusiano kati ya Russia na China ni mfano wa kuigwa wa uhusiano wa kimataifa katika karne ya 21.