Iran na Iraq kufanya duru ya tatu ya mazungumzo kuhusu uchunguzi juu ya kuuawa kwa Qasem Soleimani
2022-02-07 09:35:04| cri

Naibu mkuu wa mamlaka ya sheria ya Iran anayeshughulikia mambo ya kimataifa Kazem Gharibabadi amesema, Kamati ya pamoja ya Iran na Iraq itafanya mazungumzo ya duru ya tatu kesho tarehe 8 huko Baghdad, Iraq, ili kufanya uchunguzi juu ya kuuawa kwa kiongozi mwandamizi wa Iran Qasem Soleimani.

Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi ya anga nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq Januari 3 mwaka 2020, na kumwua kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Iran imesema mauaji hayo yamekwenda kinyume na sheria ya kimataifa ambayo ni kitendo cha kigaidi cha kimataifa.