Rais Xi ampongeza Mattarella kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Italia
2022-02-07 09:33:35| cri

Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pongezi mwenzake wa Italia Sergio Mattarella kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

Rais Xi amebainisha kuwa China na Italia ambazo zina uhusiano wa kihistoria, kuungana mkono na zenye maslahi mapana, zimeweka mfano kwa jumuiya ya kimataifa katika kuaminiana, kutafuta msingi wa pamoja wakati zikiondoa tofauti, na kuwa na ushirikiano wa kunufaishana.

Vilevile rais Xi amesema nchi hizi mbili ambazo zimepambana na COVID-19 kwa nguvu zote, zinasherehekea kwa pamoja miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Italia, na kuungana mkono katika kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan ya mwaka 2026, huku mwaka wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Italia ukikaribia kuanza, ambapo utaleta fursa nyingi za maendeleo katika uhusiano wa pande mbili.