China na Argentina zasaini makubaliano ya maelewano juu ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja
2022-02-07 09:32:33| cri

China na Argentina zasaini makubaliano ya maelewano juu ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja_fororder_中国阿根廷

China na Argentina zasaini makubaliano ya maelewano juu ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja_fororder_中阿

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili, baada ya mkutano kati ya Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Argentina Alberto Fernandez, China na Argentina zimesaini makubaliano ya maelewano juu ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Baada ya kupokea mwaliko wa China, Rais Fernandez amezuru China na kuhudhuiria sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing Ijumaa usiku. Makubaliano hayo yanayohimiza kwa pamoja ujenzi wa Uchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya Baharini ya karne ya 21 kati ya serikali ya China na serikali ya Argentina, yamesainiwa wakati mwaka huu nchi hizi mbili zinaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi.

China na Argentina zimekubaliana kuongeza uwekezaji wa pande mbili, kuzidi kukamilishana kiuchumi na kutafuta fursa mpya za kiuchumi. Taarifa imeongeza kuwa wamekubaliana kusukuma mbele maendeleo endelevu ya kijani, uwekezaji na ushirikiano kwenye uchumi wa kidijitali.