CMG yasaini makubaliano ya ushirikiano na ofisi ya kitaifa ya vyombo vya habari ya Argentina
2022-02-07 20:07:59| CRI

CMG yasaini makubaliano ya ushirikiano na ofisi ya kitaifa ya vyombo vya habari ya Argentina_fororder_src=http___img1.mydrivers.com_img_20180321_e29d07fffdda48c4b9a636580415fdc8&refer=http___img1.mydrivers

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limesaini makubaliano ya ushirikiano na Ofisi ya Katibu wa Mambo ya Kitaifa Anayeshughulikia Vyombo vya Habari ya Argentina.

Huu ni mwaka wa 50 tangu China na Argentina zianzishe uhusiano wa kibalozi, na pia ni mwaka wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Ili kutekeleza makualibano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo, na kukuza ushirikiano na mawasiliano ya watu, CMG na ofisi hiyo zitafanya ushirikiano katika kubadilishana vipindi vya matangazo, teknolojia, mawasiliano ya watu, na sekta ya kiuchumi ya uenezi.  

Ofisi ya Katibu wa Mambo ya Kitaifa Anayeshughulikia Vyombo vya Habari ya Argentina ni mamlaka ya juu zaidi ya serikali ya usimamizi wa vyombo vya habari nchini humo, na chini yake kuna Shirika Kuu la Utangazaji la Argentina, Shirika la Habari la Argentina, na Kampuni ya Habari za Umma ya Argentina.